Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Februari 05, 2023 Local time: 17:50

Melania Trump akabidhi tuzo ya ujasiri kwa wanawake 13


Mke wa rais Melania Trump na naibu waziri Shannon wakiwa na wanawake Jasiri waliopata tuzo ya mwanamke Jasiri 2017.

Nguyen Ngoc wa Nhu Quyn bloga wa Vietnam hakuweza kuhudhuria kwa sababu amehukumiwa kifungo jela.

Mke wa rais wa Marekani Melania Trump alikabidhi tuzo za mwanamke jasiri kwa wanawake 13 mjini Washington Jumatano.

“Washindi hawa nilio nao hapa wamepigania haki zao na za wengine kama vile serikali , mahakama, ugaidi, vita na rushwa alisema Melania Trump.

Nguyen Ngoc wa Nhu Quyn bloga wa Vietnam hakuweza kuhudhuria kwasababu amehukumiwa kifungo jela.

Baadhi ya wengine waliopata tuzo ni pamoja na Shamrmin Akter mwanaharakati dhidi ya ndoa za kulazimishwa kutoka Bangladesh.

Malebogo Molefhe mwanaharakati wa haki Bostwana.

Rebbeca Kabugo wa Congo mwanaharakati wa siasa na jamii katika jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, Janat Al-Ghezi mkurugenzi msaidizi wa Organization of Women’s Freedom huko Iraq, Meja Aichatou Ousmane Issaka naibu Mkurugenzi wa kazi za jamii katika hospitali ya kijeshi ya Niamey Niger. Veronica Simogun mkurugenzi na mwanzilishi wa Family for Change Association, Papua New Guinea.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG