Hijja ni nguzo ya tano katika Uislam ambayo inamlazimisha kila muislam mwanamke na mwanaume mwenye uwezo na afya njema kutekeleza ibada hiyo mara moja katika umri wake. Mahujaji hufanya safari kwenda kutekeleza ibada hiyo nchini Saudi Arabia
Msimu wa Hija : Kuwasili mahujaji Msikiti Mtukufu wa Makka
Mahojaji waanza kuwasili mjini Makka, Saudi Arabia, Jumapili kwa ajili ya kutekeleza ibada ya HIjja

1
Mahujaji wakiwa wanatufu kuzunguka eneo takatifu la Kaaba, jengo la pembe nne lilioko ndani ya msikiti mkuu wa Makka, katika mji mtukufu wa Makka, Saudi Arabia, Jumapili, Aug. 4, 2019.

2
Baadhi ya Mahujaji walipokuwa katika ibada ya Hijja Septemba 21, 2015. (Foto: AP)

3
Mahujaji wakiwa wanasubiri passi zao za kusafiria uwanja wa ndege wa Jeddah kabla ya kuanza ibada ya Hijja, Agosti 3, 2019.

4
Mahujaji wakiwa wanachukuliwa alama za vidole kabla ya kuanza ibada ya Hijja baad ya kuwasili uwanja wa ndege wa Jiddah Saudi Arabia, Jumamosi, Aug. 3, 2019