Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:14

Mlipuko wa kujitoa muhanga Mogadishu waua watu watatu


Maafisa wa usalama wakilinda eneo lililotokea mlipuko wa bomu Mogadishu, Somalia, Feb. 13, 2021.
Maafisa wa usalama wakilinda eneo lililotokea mlipuko wa bomu Mogadishu, Somalia, Feb. 13, 2021.

Gari lililokuwa na bomu la kujitoa mhanga limemuua watu watatu na kujeruhi wengine wasiopungua wanane katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu mapema Jumamosi asubuhi.

Mlipuko huo uliotokea karibu na kizuizi cha usalama pia liliharibu angalau darzeni ya magari, mamlaka husika na walioshuhudia tukio hilo wamesema.

Msemaji wa jeshi la polisi amesema dereva wa gari hilo alikaidi amri ya kusimama na wanajeshi walilirushia gari hilo risasi lilipokuwa linalazimisha kupita kwenye kizuizi kimoja kati ya vizuizi viwili.

Hakuna aliyedai kuhusika na tukio hilo. Eneo la mlipuko liko karibu na jengo la bunge na makazi ya rais.

Mlipuko huo umetokea wakati wana siasa nchini Somalia wakivutana juu ya kuitisha uchaguzi mkuu, ambao awali ulipangwa kufanyika Februari 8.

Baadhi yao wanasema kuwa Rais Mohamed Abdullahi Mohamed amejiongezea muda kuwa madarakani.

Maeneo muhimu Mogadishu mara nyingi yamekuwa yakilengwa na mashambulizi ya kikundi cha ndani cha al-Qaida – kinacho husishwa na kikundi cha kigaidi cha al-Shabab, ambacho kimejihusisha na ghasia za muda mrefu zinazo lenga kuipindua serikali ya Somalia inayo tambulika kimataifa.

Al-Shabab hivi karibuni ilitishia kushambulia vituo vya kupiga kura wakati wa uchaguzi mkuu.

XS
SM
MD
LG