Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 16:36

Wanajeshi wa Amisom, Marekani waanza mipango ya kuondoka Somalia, hali ya wasiwasi yaongezeka


Wanajeshi kutoka muungano wa Afrika - AMISOM walio nchini Somalia.
Wanajeshi kutoka muungano wa Afrika - AMISOM walio nchini Somalia.

Hali ya wasiwasi inaendelea kuongezaka Somalia kufuatia hatua ya mataifa ya nje kuanza kuondoa wanajeshi wake nchini humo baada ya miongo mitatu ya kulinda amani.

Nchi hiyo huenda ikakumbana na hali ngumu kiusalama wakati inajitayarisha kwa uchaguzi mkuu.

Somalia imekuwa ikitegemea msaada wa wanajeshi kutoka nchi zingine kwa ajili ya usalama wake tangu kaunguka kwa utawala wa Siad Barre mwaka 1991.

Nchi hiyo inakabiliwa na mashambulizi ya kila mara kutoka kwa makundi ya wapiganaji nay a kigaidi.

Wanajeshi kutoka muungano wa Afrika wanaoshika doria nchini Somalia – AMISOM, wameanza hatua za mwisho za kupokeza majukumu ya kiusalama kwa wanajeshi wa Somalia kwa matayarisho ya kuondoka nchini humo ifikapo Desemba mwaka ujao 2021, kulingana na maamuzi ya baraza la usalama la umoja wa mataifa, namba 2520.

Marekani nayo imeanza mchakato wa kupokeza majukumu kutoka kwa wanajeshi wake walio Somalia hadi kwa wanajeshi wa nchi hiyo, kwa matayarisho ya kuondoa wanajeshi wake.

Marekani hata hivyo imesema kwamba itaendelea na ushirikiano wake wa kijeshi kupambana na makundi ya kigaidi Afrika mashariki.

Wanajeshi 700 wa Marekani wamepangiwa kuondoka Somalia ifikapo Januari tarehe 15, siku tano kabla ya rais Donald Trump kuondoka Madarakani.

Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG