Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 08, 2024 Local time: 15:36

Mkuu wa Hamas: Kumuua al-Arouri ni 'kitendo cha kigaidi' na ukiukaji wa uhuru wa Lebanon


Maandamano dhidi ya mauaji ya Saleh al-Arouri huko Ramallah.
Maandamano dhidi ya mauaji ya Saleh al-Arouri huko Ramallah.

Mkuu wa Hamas Ismail Haniyeh siku ya Jumanne alisema kuuliwa kwa naibu kiongozi wa kundi la Palestina Saleh al-Arouri katika shambulio la Israel mjini  Beirut ni "kitendo cha kigaidi."

Marehemu Saleh al-Arouri
Marehemu Saleh al-Arouri

Haniyeh amesisitiza kuwa mauaji hayo pia ni ukiukaji wa mamlaka ya Lebanon na upanuzi wa uadui wa Israel dhidi ya Wapalestina.

Katika hotuba yake iliyopeperushwa kwenye televisheni, Haniyeh alimuomboleza al-Arouri na viongozi wawili wa Brigedi za Al Qassam, Samir Findi Abu Amer na Azzam Al-Aqraa Abu Ammar.

Viongozi wote hao waliuawa Jumanne usiku katika shambulio la ndege zisizo na rubani za Israel katika viunga vya Beirut kusini mwa Dahiyeh.

Israel Yatangaza kupunguza majeshi yake Gaza

Wakati huo huo mapigano makali yanaendelea katikati na kusini mwa Gaza, na kuzunguka mji wa Khan Younis na miji mingine katika eneo lenye watu milioni 2.3 huko Gaza ambao wengi wao wamekimbia. Vita hivyo vimesababisha karibu 85% ya wakazi wa Gaza kukimbia makazi yao.

Israel ilitangaza Jumatatu kwamba itaondoa wanajeshi elfu kadhaa, kutoka Gaza katika wiki zijazo.

Hata hivyo, Waziri wa Ulinzi wa Israel alisema litakuwa kosa kufikiri kwamba Israel inapanga kusitisha vita.

Mashambulizi ya anga, ardhini na baharini ya Israel huko Gaza yameua zaidi ya watu 22,100 huko Gaza, theluthi mbili kati ya hao wakiwa wanawake na watoto, kulingana na Wizara ya Afya katika eneo linalotawaliwa na Hamas. Idadi hiyo haitofautishi kati ya raia na wapiganaji.

Vyanzo vya habari hii ni mashirika ya habari ya Reuters na AP.

Forum

XS
SM
MD
LG