Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 08, 2024 Local time: 21:05

Israel kupunguza wanajeshi Gaza


Israel, imeashiria  awamu mpya ya mashambulizi yake huko Ukanda wa Gaza, kwakutangaza  Jumatatu kupunguza idadi ya wanajeshi wake huko Gaza huku ikiendelea na operesheni za kuilenga  Hamas katika eneo hilo.

Taarifa ya jeshi la ulinzi la Israel, imesema kuwa kuondoka kwa wanajeshi hao kutapunguza kwa kiasi kikubwa mzigo wa uchumi na kuruhusu wanajeshi kujipanga na kuongeza nguvu kwa operesheni zijazo, huku mapigano yakiendelea na huduma zao zitaendelea kuhitajika.

Israel, pia iliondoa vifaru vyake vya kivita kutoka katika baadhi ya wilaya za Gaza, kwa mujibu wa wakaazi wa huko.

Waziri wa ulinzi wa Israel, Yoav Gallant, amesema katika mkutano na wanahabari Jumatatu kwamba baadhi ya jamii za Israel kaskazini mwa Ukanda wa Gaza ambazo zilihamishwa kufuatia shambulio la Oktoba 7 lililofanywa na Hamas, zitarejea hivi karibuni wakati operesheni za kijeshi zikiendelea.

Forum

XS
SM
MD
LG