Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 20:49

Mkutano wa viongozi wa Marekani na Afrika wajadili mustakbali wa vijana


Mkutano wa viongozi wa Marekani na Afrika unaofanyika mjini Washington, DC, Marekani. Jumatano Desemba 14, 2022.
Mkutano wa viongozi wa Marekani na Afrika unaofanyika mjini Washington, DC, Marekani. Jumatano Desemba 14, 2022.

Mkutano wa Marekani na Afrika ulianza Jumanne katika mji mkuu wa Marekani kukiwa na ajenda mbali mbali.

Masuala ambayo yalianzia hali ya hewa na nishati, kipindi cha mpito cha amani, ulinzi na utawala bora.

Kwenye mojawapo ya vikao hivyo suala la vijana wa kiafrika na jukumu la wanadiaspora lilijadiliwa kwa kina zaidi.

Karibu viongozi 50 wamekaribishwa na Rais Joe Bideni – kuanzia marais mpaka mawaziri wakuu na mawaziri wa mambo ya nje na mkuu wa Umoja wa Afrika – waliwasili mapema wiki hii.

Mkutano wa Marekani na Afrika
Mkutano wa Marekani na Afrika

Makamu rais wa Marekani Kamala Harris alianza mkutano huo kwa kuhudhuria kikao maalum ambacho kilizungumzia kuhusu viongozi vijana wa kiafrika na wale ambao wanaishi nje ya bara hilo.

“Naamini kwa dhati kabisa kwamba ubunifu na werevu wa viongozi vijana Afrika utasaidia kubadili mustakbali wa dunia. Na mawazo yao, mawazo yenu, uvumbuzi na juhudi utainufaisha dunia nzima. Utawala wa Biden na Harris una azma ya kuwepo huko pamoja na nyinyi, viongozi hawa vijana wanafahamu kwamba ni hamasa, azma ya vijana ambayo itatusukuma na kutupeleka mbele,” amesema Kamala Harris.

Makamu rais alitangaza utawala utawekekeza ziada ya dola milioni 100 ili kupanua Mpango wa viongozi vijana maarufu kama YALI na benki ya Export – Import Marekani ilikuwa inaingia katika makubaliano mapya ya maelewano ambayo yatafungua njia kwa ufadhili wa kibiashara wa takriban dola bilioni moja huko barani Afrika.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akikutana na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed wakati wa mkutano wa viongozi wa Marekani na Afrika katika Ukumbi wa Convention Center mjini Washington DC, Desemba 13, 2022.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akikutana na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed wakati wa mkutano wa viongozi wa Marekani na Afrika katika Ukumbi wa Convention Center mjini Washington DC, Desemba 13, 2022.

Baadaye, Waziri wa Mambo ya Nje, Antony Blinken aliungana na Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin na Mkuu wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa, Samantha Power katika moja ya mikutano kujadili amani, utawala bora na usalama na marais wa Niger, Msumbiji na Somalia, na Moussa Faki Mahamat, mwenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika.

Blinken amesema “Hakuna mfano hata mmoja juu ya kujenga taasisi imara. Nadhani lazima tujulishane kila mmoja. Lazima tufahamu hali ilivyo maeneo husika, na mahitaji ya huko na kutokana na mtizamo wa Marekani, hii pi ni kuhusu ushindani na wengine. Hii haihusu kuwaambia marafiki na washirika wetu, mnatakiwa mchague. Hii inahusu kuwapa maamuzi ya kweli, kuwapa ushirika wa kweli, na matumaini ya kujenga pamoaj ushindani kulekea juu, siyo ushindani kwenda chini.”

Waziri wa Ulinzi wa Marekani alisema “tunataka kuelewa kitu gani muhimu sana kwenu. Na tukienda mbele zaidi, tunataka kuhakikisha kwamba tunafanya mambo ya maendeleo na uwezeshaji kwa majeshi yetu ya usalama na kuwasaidia kufanya kazi kwenye ulinzi wa mifumo yenu kwa njia ambayo itawanufaisha, na kwa hakika kuhamasisha uthabiti wa kikanda.”

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani (katikati) akihudhuria utiaji saini wa Makubaliano ya Kikanda na marais wa Benin, Patrice Talon (kushoto) na Niger, Mohamed Bazoum (kulia), wakati wa mkutano wa viongozi wa Marekani na Afrika, mjini Washington DC, Desemba 14, 2022.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani (katikati) akihudhuria utiaji saini wa Makubaliano ya Kikanda na marais wa Benin, Patrice Talon (kushoto) na Niger, Mohamed Bazoum (kulia), wakati wa mkutano wa viongozi wa Marekani na Afrika, mjini Washington DC, Desemba 14, 2022.

Mahamat alisema Marekani inatoa msaada kwa nchi kama vile Niger, Msumbiji, Somalia na Chad. Lakini pia alielezea kwamba majeshi ya Afrika bado hayana vifaa vya kutosha.

“Hakuna anayesikiliza vilio vya Afrika wakati linapokuja suala la kuongezeka kwa janga hili,” amesema Mahamat.

Rais wa Niger Mohammed Bazoum alisema wamelikabili janga hilo, hivyo wanahitaji kuchukua hatua mbali mbali. Kwanza ni uhamasishaji, licha ya yote, na hasa kwa sababu hizo, kwa vile tuna changamoto mbele yetu, kwahiyo ni vyema kuhamasisha demokrasia, kuhamasisha utawala wa sheria, kuhamasisha heshima kwa haki za binadamu.

Sikya pili ya mkutano huo Jumatano viongozi wa Afrika walilenga zaidi katika kusukuma mbele ushirikiano wa pande wa kibiashara na uwekezaji, ambayo utaboresha jukumu la Afrika katika uchumi wa dunia na kusukumba mbele sekta muhimu.

XS
SM
MD
LG