Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 30, 2022 Local time: 03:57

Mke wa Miguna Miguna aelezea kufukuzwa mumewe Kenya


Miguna Miguna

Wakili wa Kenya Miguna Miguna ametolewa nchini Kenya kwa nguvu na kurejeshwa Canada baada ya kukamatwa mwisho wa wiki, mke wake Jane Miguna amesema.

Mkewe ameeleza kuwa hata hivyo mumewe alikuwa anajitayarisha kurudi Canada katika mahojiano na gazeti la Canada, Macleans, masaa machache baada ya mumewe kuondolewa kwa nguvu jijini Nairobi.

Mwanasiasawa Umoja wa upinzani wa Nasa ambaye ni shupavu alisafirishwa kwenye ndege iliyokuwa inaelekea Amsterdam na kuelekea Canada Jumanne (Februari 6) usiku, mawakili wake wamesema.

Serikali, imetetea kitendo chake cha kumwondosha Miguna nchini, na kusema wakili huyo alikuwa ameukana uraia wake na alikuwa hajatoa taarifa kuwa ana uraia wa Canada.

Katika mahojiano yake ambayo yamechapishwa katika tovuti ya gazeti hilo, mkewe Miguna amesema kuwa mumewe, ambaye alikamatwa na polisi Ijumaa [2 Februari] akiwa nyumbani kwake Runda [makazi yaliyoko katika kitongoji cha Nairobi], aliwafahamisha watoto wake watatu kuwa alikuwa amepanga kurudi nyumbani.

Watoto wake, amesema walikuwa wanamtarajia baba yao kuwasili mwisho wa wiki lakini hakuonekana, na juhudi zake za kufuatilia ziligonga ukuta.

"Walikuwa wanamtarajia baba yao kurudi mwisho wa wiki. Hivi sasa wamekuwa wananiuliza kwa nini baba hajarejea nyumbani, na mimi nawaambia kuwa anaudhuru," amesema.

Na ilivyokuwa kwamba alikuwa hataki kuwapa watoto wasiwasi, mama huyo hakuwafahamisha watoto wake kuwa baba yao alikuwa amekamatwa.

Amesema kuwa alifanya bidi kumtafuta Miguna kwa siku kadhaa na kupiga simu kwa mshitukomkubwa akiwasiliana na ubalozi wa Canada nchini Nairobi baada ya polisi kushindwa kumleta Miguna mahakamani kwa amri iliyotolewa.

“Tangu Jumapili mpaka jana Jumanne, nilikuwa sijaweza kupata taarifa iwapo Miguna yuko hai au amekufa,” Mke wa Miguna alisema.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG