Sullivan yuko katika ziara huko Mashariki ya Kati kuzungumzia masuala muhimu ya ukanda huo pamoja viongozi wa nchi mbali mbali.
Taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Misri mjini Cairo, inaeleza kwamba Rais el-Sisi na Sullivan walizungumzia pia suala la ujenzi wa Ukanda wa Gaza, mvutano kuhusu bwawa la Ethiopia kwenye mto wa Blue Nile Gerd uhusiano kati ya Marekani na Misri na hali nchini Tunisia Yemen na Iraq.
Taarifa hiyo haikuelezea kama viongozi hao wawili walizungumzia masuala ya haki za binadamu ambayo White House ilieleza Jumanne kuwa litakuwa kwenye ajenda ya mazungumzo wakati wa ziara ya Sullivan.
Kwa mujibu wa Libya pande zote mbili zimekubaliana kuimarisha ushirikiano wa kuondolewa wanajeshi na wapiganaji wakigeni na kunganishwa pamoja taasisi zote za jeshi la Libya. Rais el-Sisi alisisitiza pia juu ya haja ya utekelezaji wa mpango wa mpito na kufanyika kwa uchaguzi mwezi wa Disemba kulingana na taarifa hiyo ya ikulu.
Uchaguzi huo ni sehemu ya juhudi zinazo ongozwa na Umoja wa Mataifa kuiunganisha tena Libya baada ya karibu ya miaka 10 ya mapigano na migawanyiko lakini bado nchi inakabiliwa na changamoto nyingi kulingana na wataalamu.
Sullivan aliwasili Cairo baada ya ziara yake ya Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu akiwa anafuatana na Brett Mcgurk mratibu wa masuala ya Mashariki ya Kati na Afrika kaskazini kwenye White House, ambako alikuwa na mazungumzo juu ya hali nchini Yemen.