Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Septemba 28, 2023 Local time: 07:58

Misri : Meli zaanza kupita katika Mfereji wa Suez


Meli ya Ever Given, imeweza kuelea katika Mfereji wa Suez, Misri ikitoa nafasi kwa meli nyingine kupita Machi 29, 2021.

Meli ya MV Ever Given imeelea tena na mfereji wa Suez umefunguliwa Jumatatu, ikiwa imeleta afueni kufuatia takriban wiki nzima tangu meli kubwa iliyobeba kontena kukwama na kukwamisha mfumo mkubwa wa usafirishaji wa bidhaa za biashara duniani.

Mwandishi wa AFP ameshuhudia wafanyakazi wa boti ndogo wakipiga honi kusheherekea baada ya meli ya Ever Given, ya mizigo yenye urefu wa viwanja vinne vya mpira wa miguu, ikisogea kutoka ukingoni mwa Suez.

Bei za mafuta zilirejea hali ya kawaida kufuatia habari za kufunguka tena mlango unaounganisha bahari ya Mediterranean na bahari ya Sham ambapo zaidi ya asilimia 10 za bidhaa za biashara ulimwenguni zinapita hapo.

Mkuu wa Mamlaka ya Mfereji wa Suez , SCA, Admirali Osama Rabie, mnamo majira ya saa tisa mchana Misri “alitangaza meli zimeanza kupita katika Mfereji huo,” mamlaka hiyo imesema katika tamko lake.

Hata hivyo, mamlaka hiyo imeeleza kuwa itachukuwa zaidi ya siku tatu kuweza kuondoa msongamano wa meli zilizokuwa zimeshindwa kupita zikiwa zinasubiri mwisho wa eneo la Mfereji upande wa kaskazini na Kusini.

Hadi kufikia hapa ambapo meli hiyo iliyokwama kuanza kuelea kulikuwa na meli 425 zikisubiri kupita.

XS
SM
MD
LG