Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 05:39

Minneapolis yatangaza hali ya dharura kufuatia ghasia kutokana na kuuawa Floyd


Kumbukumbu ya George Floyd
Kumbukumbu ya George Floyd

Meya wa Minneapolis Jacob Frey ametangaza hali ya dharura katika mji uliojaa mvutano ambako mmarekani mweusi aliuwawa alipokuwa chini ya ulinzi wa polisi Jumatatu usiku.

Wakati huo huo gavana wa Minnesota Tim Walz ametoa wito kwa walinzi wa kitaifa kujaribu kuzuia usiku mwingine wa tatu wa vurugu.

Wanajeshi 500 wameitwa kutoa ulinzi huko katika miji ya Minneapolis, St Paul na jamii zinazozunguka.

Maduka kadhaa huko Minneapolis na mji pacha wa St. Paul yalichomwa moto Alhamisi usiku.

Maafisa wa polisi wa St Paul wanaripoti kuwa maafisa wake wamepigwa na mawe pamoja na chupa.

George Floyd aliyefariki baada ya polisi kumkandamiza shingoni huku akiwa amefungwa pingu baada ya maafisa wa polisi kumweka chini ya ulinzi katikati ya barabara wiki hii mjini Minnessota.

Kufa kwa Floyd kulisababisha Maandamano na ghasia huko Minneapolis na kikosi cha kitaifa cha ulinzi kilipelekwa kulinda amani.

Maandamano hayo yalisamba katika majimbo mengine huku maandamano yakiendelea katika majimbo ya Memphis, New York,California, Chicago, Okaland, Ohio na Colorado.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC

XS
SM
MD
LG