Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 17:28

Mgomo kudai nyongeza ya mishahara wasitisha usafiri wa umma Ujerumani


Usafiri wa umma wasimama kufuatia mgomo wa wafanyakazi Ujerumani.
Usafiri wa umma wasimama kufuatia mgomo wa wafanyakazi Ujerumani.

Treni , ndege na mifumo ya usafiri wa umma ilisimama katika sehemu nyingi nchini  Ujerumani Jumatatu wakati vyama vya wafanyakazi vilipoitisha mgomo mkubwa wa siku moja kuhusu mishahara.

Mgomo huu ni katika juhudi za kushinda mfumuko wa bei uliongezeka kwa wanachama wake.

Maandamano ya saa 24 pia yaliathiri usafirishaji wa mizigo kwa njia ya reli na meli wakati wafanyakazi wa bandari na njia za majini wakijiunga katika mgomo huo.

Vyama vya wafanyakazi vinataka nyongeza ya mshahara kwa takriban asilimia 10.5 na vimekataa nyongeza ya asilimia 5 kutoka kwa waajiri kwa awamu mbili pamoja na malipo ya mara moja.

Volker Geyer, Naibu mwenyekiti wa shirikisho la DBB ( muungano wa watumishi wa umma ujerumani) anaeleza: “ Tunadai asilimia 10.5 ambayo ni sawa na dola 540 . Na kiasi hiki cha chini pia ni muhimu sana kwetu. Kwa sababu ni makundi ya watu wa kipato cha chini na kati ambayo yameathiriwa sana na mfumuko wa bei .”

Kampuni ya Reli ya Dochi Ban iliyataja madai ya chama hicho kuwa yametiwa chumvi na kuonya kuwa mamilioni ya wasafiri wataathirika.

Tiketi za treni ambazo haziwezi kutumika kwa sababu ya kuvurugika kw usafiri zitaendelea kutumika na wasafiri wanapaswa kuangalia tovuti ya kampuni hiyo ili kupata maelezo zaidi.

Habari hii inatokana na mashirika mbalimbali ya habari.

XS
SM
MD
LG