Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 06, 2024 Local time: 01:56

Mdahalo: Len Pen amkosoa hasimu wake Macron kwa kuangazia Ulaya


Mgombea urais Emmanuel Macron, kushoto, na mgombea urais wa mrengo mkali wa kulia Marine Le Pen pose kabla ya kuanza mdahalo wao Paris, April 20, 2022.
Mgombea urais Emmanuel Macron, kushoto, na mgombea urais wa mrengo mkali wa kulia Marine Le Pen pose kabla ya kuanza mdahalo wao Paris, April 20, 2022.

Rais Emmanuel Macron amechuana uso kwa uso katika mdahalo wa kipekee wa televisheni na mpinzani wake wa mrengo mkali wa kulia Marine Le Pen kuhusu kupungua kwa ushawishi wa nchi hiyo barani Afrika.

Le Pen alianza kumkosoa Macron kwa kuangazia zaidi Ulaya na sio dunia.

“Ufaransa imekuwa nchi ya bara hili, sisi ni nguvu ya kimataifa na tunahitaji kuangalia upya matarajio yetu ya ushawishi wa kimataifa, kufanya kazi pamoja na washirika maalumu hasa nchi zinazozungumza kifaransa huko Afrika, ambao ni washirika wa muda mrefu wa Ufaransa.

Tunahitaji kurejesha upya ushirikiano wetu , alisema.” Macron alijibu kwa kusisitiza juhudi za kurekebisha uhusiano na makoloni ya zamani na kueleza urithi wa ukoloni.

“ Nimekuwa Afrika kuliko watangulizi wangu wote . Ninathamini uhusiano huu. Niliuanzisha tena, niliuzindua tena na nimekuwa mwaminifu na jasiri kuhusu historia yetu, alisema.

Hali ya Ufaransa kutokuwa maarufu Afrika inazidi kuongezeka kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa kwa miongo kadhaa, licha ya Macron kuongeza misaada , kushawishi kurejeshwa kwa vito vya thamani vya kitamaduni vilivyoibwa wakati wa vita vya kikoloni na kufanya juhudi kuwahusisha vijana na jumuiya za kiraia.

XS
SM
MD
LG