Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 11:59

Rais wa zamani wa Ufaransa Francois Hollande aomba Wafaransa kumpigia kura Emmanuel Macron.


Rais Emmanuel Macron akiandamana na rais wa zamani Francois Hollande wakati akiondoka Ikulu mjini Paris baada ya sherehe za kuapishwa rais mpya, Mei 14, 2017. Picha ya AP.
Rais Emmanuel Macron akiandamana na rais wa zamani Francois Hollande wakati akiondoka Ikulu mjini Paris baada ya sherehe za kuapishwa rais mpya, Mei 14, 2017. Picha ya AP.

Rais wa zamani wa Ufaransa wa siasa za Kisocialist Francois Hollande Alhamisi ametoa wito kwa wapiga kura kumuunga mkono Emmanuel Macron katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais tarehe 24 Aprili.

“Mimi ni rais wa zamani wa Ufaransa na ninajua kuwa katika uchaguzi muhimu kama huu, kilicho muhimu ni Ufaransa, mshikamano wake, mustakabali wake wa Ulaya na uhuru wake. Hii ndiyo sababu ninatoa wito kwa Wafaransa kumpigia kura Emmanuel Macron,” Hollande ameiambia televisheni ya TF1.

Ameongeza kuwa “Kura ya Macron itahakikisha Marine Le Pen hapati ushindi.”

Zikisalia siku 10 kabla ya duru ya pili ya uchaguzi ambayo itaamua nani ataongoza taifa hilo la pili la Umoja wa Ulaya lenye uchumi mkubwa katika miaka mitano ijayo, kura ya maoni inaonyesha kwamba Rais Emmanuel Macron mwenye siasa za mrengo wa kati anaongoza kidogo dhidi ya hasimu wake wa siasa kali za mrengo wa kulia Marine Le Pen.

Mwaka 2016, Hollande alipata viwango vya chini sana kuhusu maoni juu ya utendaji kazi wake, na aliamua kutogombea muhula wa pili.

XS
SM
MD
LG