Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 12:28

Rais Macron afanya kampeni kaskazini ya Ufaransa


Rais Emmanuel Macron akiongea na wafuasi wake huko Spezet, Brittany, Jumanne, April 5, 2022.
Rais Emmanuel Macron akiongea na wafuasi wake huko Spezet, Brittany, Jumanne, April 5, 2022.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amekutana na wakaazi wa mji wa kaskazini wa Denain Jumatatu ambako mpinzani wake wa mrengo wa kulia Marine Le Pen amepata zaidi ya asilimia 41 ya kura.

Idadi hii inalinganishwa na za Macron kwa asilimia 14 katika duru ya kwanza ya uchaguzi.

Macron amekutana na wakaazi wa mji huo wengi wao wamepinga mapendekezo yake ya mabadiliko ya malipo ya uzeeni akiongeza umri wa kustaafu kutoka miaka 62 hadi 65.

Mbunge wa Denain, Anne Lise Dufour Tonini, aliwaambia waandishi wa habari atampigia kura Macron bila kusita katika duru ya pili ya uchaguzi lakini analengo la kutoa shinikizo kwake kusukuma zaidi mapendekezo ya mrengo wa kushoto.

Kutokana na kura nyingi za wagombea 12 kwenye duru ya kwanza zilizohesabiwa leo asubuhi, Macron amepata zaidi ya asilimia 27 na Le Pen amepata asilimia 23.

Mgombea Jean Luc Melenchon ameshika nafasi ya tatu kwa asilimia 22.

XS
SM
MD
LG