Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 03:27

Mawaziri 5 wahusishwa na kashfa ya mikataba mibovu


Bunge la Tanzania
Bunge la Tanzania

Kashfa mpya inayo wahusisha mawaziri watano wazamani imeibuka katika ripoti ya moja ya kamati mbili maalum za Bunge la Tanzania, zilizoundwa kuchunguza masuala ya mikataba mibovu inayodaiwa kuwa imeisababishia hasara serikali.

Ripoti hiyo imewataja Daniel Yona, Maokola Majogo, marehemu Abdallah Kigoda, Nazir Karamagi na William Ngeleja ambao wote kwa vipindi tofauti waliwahi kutumikia iliyokuwa Wizara ya Nishati na Madini.

Wakati kamati hizo zilizoundwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai, zikiwasilisha ripoti hiyo majina ya mawaziri hao yaliwekwa bayana.

Wachambuzi nchini Tanzania wamesema kuwa kutajwa kwa Ngeleja, Yona na Karamagi, ni katika mtiririko wa kashfa zilizoelekezwa dhidi ya mawaziri hao.

Ngeleja ambaye pia ni Mbunge wa Sengerema kupitia CCM, ni mara ya tatu kutajwa kuhusiana na kashfa.

Mara ya kwanza alihusishwa na ufisadi wa fedha za Escrow, akinufanika na mgawo wa sh milioni 40.4 ambazo baadae alizirudisha.

Alitajwa pia katika ripoti ya tume iliyoundwa kuchunguza mfumo wa uchimbaji, udhibiti, usimamizi na umiliki wa madini ya almasi na Tanzanite, akidaiwa kuhusika na dosari zilizoisababisha nchi kupoteza fedha nyingi.

Yona ambaye alikuwa Waziri wa Nishati na Madini wakati wa utawala wa awamu ya tatu, amekuwa akinyoshewa kidole kwa kashfa mbalimbali, ikiwamo ya ufisadi wa matumizi mabaya ya rasilimali za umma.

Aliwahi kudaiwa kuuza kinyemela sehemu yenye utajiri mkubwa wa makaa ya mawe, Kiwira kwa Kampuni ya Tan – Power Resources (TPR).

XS
SM
MD
LG