Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 13, 2024 Local time: 13:54

Mawaziri wa Fedha wa G7 watathmini athari za vita vya Russia na Ukraine


Waziri wa Fedha wa Ujerumani Christian Lindner
Waziri wa Fedha wa Ujerumani Christian Lindner

Mawaziri wa Fedha katika  kundi la G7, nchi zinazoongoza kiuchumi, wamekutana Alhamisi ambapo watazungumzia  matokeo ya haraka ya vita vya Russia na Ukraine na janga la COVID- 19.

Katika mkutano huo watajadili mipango yao kwa mageuzi ya uchumi wa dunia.

Mgogoro wa wakimbizi, mfumuko mkubwa wa bei, ukosefu wa usalama wa chakula unaochangiwa na vita na mabadiliko ya hali ya hewa na athari za janga la miaka mingi ni maswala machache yanayowavuta viongozi hao katika mkutano huo.

Waziri wa Fedha wa Ujerumani Christian Lindner, anayesimamia mkutano huo, anasema ana matumaini kwamba nchi zinazoongoza kwa demokrasia duniani zinaweza kukubaliana kwa ufadhili zaidi kwa ajili ya Ukraine wakati inajitetea dhidi ya Russia.

Lindner amewaambia waandishi wa habari kabla ya mkutano huo wa Mawaziri wa Fedha wa G7 huko Koenigswinter, Ujerumani kwamba Ukraine itahitaji mabilioni ya Euro, katika miezi ya karibuni.

Ukosefu wa usalama wa chakula umekuwa ni suala kuu la majadiliano hata kabla ya mkutano kuanza.

Siku ya Jumatano Marekani na maafisa wengine walianzisha mpango wa mabilioni ya dola kushughulikia hatari hiyo inayoukumba uchumi wa dunia unaozidi kuwa tete.

XS
SM
MD
LG