Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 16:32

Marekani na mataifa ya G7 waafikiana kupiga marufuku ununuzi wa mafuta ya Russia


Wafanyakazi wakipita kwenye tenki la kuhifadhia mafuta la Kaleikino katika jimbo la Transneft, Russia, April 27, 2022. Picha ya Reuters
Wafanyakazi wakipita kwenye tenki la kuhifadhia mafuta la Kaleikino katika jimbo la Transneft, Russia, April 27, 2022. Picha ya Reuters

Marekani na mataifa mengine yenye uchumi mkubwa duniani yanayounda kundi la G7 yaliyokutana Jumapili yameafikiana kupiga marufuku au kutonunua mafuta ya Russia, yakilenga moja ya chanzo kikubwa cha mapato ya Moscow kama njia ya kuiadhibu Russia kwa kuivamia Ukraine kwa wiki 10 sasa.

“Hii itakuwa na athari kubwa kwa uchumi wa Rais Vladimir Putin na kumnyima mapato anayoyahitaji kufadhili vita vyake,” viongozi wa G7 kutoka Uingereza, Canada, Ufaransa, Ujerumani, Italy, Japan na Marekani wamesema baada ya mkutano kwa njia ya mtandao na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky.

Marekani ilikuwa tayari imesitisha kununua mafuta ya Russia, wakati nchi 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya, ambazo zinanunua robo ya mafuta ghafi ya Russia, zilitangaza mipango ya kusitisha kununua mafuta hayo. Nchi hizo zinaendelea na mazungumzo ili kutafakari namna ya kutoendelea kutegemea mafuta ya Moscow.

Mkutano huo na Zelensky umefanyika siku ambapo viongozi wa G7 wameadhimisha kumalizika kwa vita vya pili vya dunia huku Russia ikijiandaa nayo leo Jumatatu kufanya maadhimisho ya kila mwaka ya ushindi wa umoja wa Soviet dhidi ya Ujerumani ya Wanazi mwaka 1945, ikiita siku ya ushindi.

​
XS
SM
MD
LG