Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 31, 2024 Local time: 01:13

Wanajeshi 957 wa Ukraine wamejisalimisha wiki hii; inasema wizara ya ulinzi Russia


Wanajeshi wa Ukraine wakiwa juu ya kifaru kufuatia mapigano yanayoendelea huko
Wanajeshi wa Ukraine wakiwa juu ya kifaru kufuatia mapigano yanayoendelea huko

Wizara ya ulinzi ya Russia ilisema Jumatano kwamba wanajeshi 959 wa Ukraine wamejisalimisha wiki hii katika ngome ya mwisho kwenye mji wa bandari uliozingirwa wa Mariupol.

Msemaji wa wizara aliwaambia waandishi wa habari kwamba idadi hiyo ilijumuisha wanajeshi 694 ambao walijisalimisha katika muda was aa 24 zilizopita. Maafisa wa Ukraine hawajathibitisha idadi hiyo.

Naibu waziri wa ulinzi wa Ukraine, Anna Malyar alisema Jumatatu kwamba zaidi ya wapiganaji 260 waliondoka kwenye magofu ya kiwanda cha chuma cha Azovstal na walijisalimisha wenyewe kwa vikosi vya Russia kulingana na idadi iliyotolewa na Russia.

Russia iliiita operesheni hiyo kuwa ni kujisalimisha kwa umma. Wa-Ukraine kinyume chake walisema ngome yake ilikuwa imekamilisha misheni yake. Lengo lilikuwa kwamba watu wetu ambao wanalinda jiji kishujaa na kumzuia adui moja kwa moja huko Mariupol, hawakuwaruhusu kupitia Mariupol, meya wa Mariupol Vadym Boychenko,aliiambia idhaa ya Ki-Ukrain ya VOA.

Wameliokoa taifa. Waliruhusu vikosi vya jeshi la Ukraine kujiandaa, na miji mingine kujiandaa zaidikwa vita hivi vibaya ambayo tayari vimetokea huko Ukraine.

XS
SM
MD
LG