Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 06:08

Mawakili wa Afrika Kusini wadai kutotendewa haki Tanzania


Sibongile Ndashe
Sibongile Ndashe

Mawakili watatu wa Afrika Kusini waliokuwa wamekamatwa nchini Tanzania wakituhumiwa kwa kukuza mapenzi ya jinsia moja wamesema hawakuwa na hatia.

Mawakili hao wa utetezi wa haki za binadamu (LHR) wenye makao yao makuu Afrika Kusini walikamatwa wakiwa pamoja na watu wengine katika hoteli moja mjini Dar es Salaam. Serikali ya Tanzania imewaondoa mawakili hao nchini.

Sibongile Ndashe, mmoja wa mawakili hao ameviambia vyombo vya habari Jumamosi kuwa polisi nchini Tanzania walikuwa hawana haki ya kuwakamata na ameishtumu mamlaka ya Dar es Salaam kwa kutowatendea haki.

Sanja Bornman wa LHR- Progamu ya Usawa wa Kijinsia amesema, “ Hakuna msingi wa sheria yoyote uliotumika katika kuwakamata watu hawa, na pia kuwapa dhamana na baadae kuifuta.

Ameongeza, "Hili linaonyesha ni jaribio la kuwadhibiti na kuwatishia watu na mawakili wanaotetea haki za binadamu, ambao kisheria walikuwa wanapata maelekezo kutoka kwa wateja wao kwa ajili ya kuchukua hatua za kisheria."

"Jambo hili halikubaliki na ni kinyume na majukumu ya kulinda haki za kibinadamu katika nchi ya Tanzania na kimataifa. Hivyo tunataka vyombo vya serikali kuwaachia huru wale wote waliokamatwa wakiwemo wanaharakati wenzetu wa Afrika Kusini," amesisitiza Bornman.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari nchini Tanzania waandalizi wa mkutano huo wamesema kuwa mkutano ulikuwa kwa ajili ya kujadili maamuzi ya serikali ya Tanzania unaohusu kuzuia utoaji wa baadhi ya huduma za afya.

Serikali mwaka huu ilisimamisha huduma za kliniki kibinafsi zinazotoa huduma za ugonjwa wa HIV na ukimwi ikidai zinajihusisha na kukuza mapenzi ya jinsia moja ambayo ni ukiukaji wa sheria za Tanzania.

Mawakili wa utetezi wa haki za binadamu (LHR) wenye makao yao makuu Afrika Kusini, walishtushwa na kitendo cha kukamatwa kwa wanaharakati wa haki za binadamu 13 wakiwemo raia wawili wa Afrika Kusini, nchini Tanzania kwa tuhuma za kufagilia mapenzi ya jinsia moja.

Kwa mujibu wa Shirika la Haki za Binadamu Amesty International, ushoga ni kinyume cha sheria katika nchi 38 kati ya nchi za Kiafrika 54 na adhabu yake ni kifo huko Mauritania, Somalia na Sudan.
Uganda in 2014 tried to impose the death penalty on those found guilty of being homosexual, however the controversial law was later repealed.

Uganda mwaka 2014 ilijaribu kuweka adhabu ya kifo kwa wale watakao kutinakana na kosa la kujihusisha na ushoga , lakini sheria hiyo tata iliondolewa kabisa siku za usoni.

XS
SM
MD
LG