Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 28, 2024 Local time: 05:03

Maseneta zaidi wajitokeza kuukubali mkataba wa Iran wa nyuklia


Seneta Cory Booker, m-Democrat jimbo la New Jersey ni miongoni mwa wanaounga mkono mkataba wa nyuklia wa Iran
Seneta Cory Booker, m-Democrat jimbo la New Jersey ni miongoni mwa wanaounga mkono mkataba wa nyuklia wa Iran

Baadaye wiki hii wabunge wa Marekani watarudi Washington baada ya mapumziko ya mwezi mmoja. Siku za karibuni zimeonekana kuwa na taarifa mbali mbali kutoka kwa maseneta kutangaza msimamo juu ya mkataba wa kimataifa wa nyuklia na Iran.

Hatua hiyo inauungaji mkono wa kutosha kuweza kuendelea, lakini bado upungufu wa uungaji mkono unaotakiwa ili kulizuia bunge kupitisha azimio la awali la kutoukubali. Kama walivyo wa-Democrat wengi, Seneta Chris Coons wa Delaware hana hamasa kubwa kuhusu mkataba wa nyuklia wa Iran. Alisema “kiukweli huu sio mkataba niliokuwa na matumaini nao. Nina wasi wasi kuhusiana na tabia za zamani za Iran za kuibia kwenye mikataba ya nyuklia”. Lakini kama walivyo wa-Democrat wengi bwana Coons bado anauunga mkono. Alisema “hatuwezi kuiamini Iran lakini mkataba huu umeegemea katika kutoaminiana, uthibitisho, kuzuia makosa yasitendeke na msimamo thabiti, diplomasia ya kimataifa, vinatupa sisi fursa nzuri ya kuizuia Iran kutoendelea na utengenezaji wa silaha za nyuklia”.

Katika siku za karibuni, maseneta watano wengine wa Democrat walitoa taarifa zinazoshabihiana za kuunga mkono licha ya mashaka yao. Seneta Cory Booker wa New Jersey alisema “ni bora kuunga mkono mkataba huu japokuwa njia zake sio nzuri hivyo”. Seneta Mark Warner wa Virginia alisema “japokuwa nimechagua kuunga mkono mkataba huu, sijaridhishwa nao”.

Seneta Chuck Schumer, m-Democrat kutoka New York
Seneta Chuck Schumer, m-Democrat kutoka New York

Hadi Ijumaa ni m-Democrat mmoja pekee seneta Chuck Schumer wa New York alitangaza kuupinga mkataba huu. Tangu wakati huo aliungana na maseneta Ben Cardin wa Maryland na Robert Menendez wa New Jersey ambao walielezea mipango yao ya kuupigia kura ya “hapana” mkataba huu.

XS
SM
MD
LG