Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 04:19

Barbara Mikulski aunga mkono mkataba wa nyuklia wa Iran


Seneta Barbara Mikulski, ni m-Democrat katika jimbo la Maryland.
Seneta Barbara Mikulski, ni m-Democrat katika jimbo la Maryland.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry aliuomba umma wa wa-Marekani kuunga mkono mkataba wa nyuklia wa Iran. “Ninaamini kulingana na uzoefu wa muda mrefu katika maisha, kwamba mkataba wa nyuklia wa Iran ni hatua kubwa sana yenye matumaini”, alisema Kerry katika hotuba yake ya Jumatano kwa kundi moja ambalo lilijumuisha taasisi za kidini na wanafunzi huko Philadelphia, Marekani.

Mjini Washington, seneta m-Democrat, Barbara Mikulski wa jimbo la Maryland, alitangaza kwamba ataunga mkono mkataba huo, unaojulikana kama Joint Comprehensive Plan of Action-JCPOA, anakuwa seneta wa 34 kufanya hivyo.

Matamshi yake ya Jumanne ni muhimu kwa sababu yanampa Rais Barack Obama idadi inayohitajika ya kuendelea na kura yake ya turufu dhidi ya azimio lolote linalopinga mkataba huo. Wa-Democrat katika bunge walisema pia watakuwa na kura za kutosha kuzuia jaribio lolote la kubadili kura ya turufu ya rais.

Msemaji wa White, Josh Ernest
Msemaji wa White, Josh Ernest

Msemaji wa White House alisema utawala unashawishika na idadi ya karibuni ya maseneta ambao wamesema wataunga mkono mkataba wa nyuklia. “Pale idadi inapokuwa juu kama hivi, kila kura ni muhimu”, alisema Josh Ernest.

Bunge linatarajiwa kujadiliana juu ya mkataba huo mwezi ujao katika siku zake 60 za kipindi cha kutathmini kabla ya kuendelea na upigaji kura wa kuukubali au kuupinga mkataba huo.

XS
SM
MD
LG