Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 01, 2023 Local time: 06:49

Seneta Merkley aunga mkono mkataba wa nyuklia wa Iran


Senata Jeff Merkley, m-Democrat kutoka Oregon, anaunga mkono mkataba wa kimataifa wa kuzuia Iran kutengeneza silaha za nyuklia
Senata Jeff Merkley, m-Democrat kutoka Oregon, anaunga mkono mkataba wa kimataifa wa kuzuia Iran kutengeneza silaha za nyuklia

Seneta mwingine wa Marekani, M-democrat, Jeff Merkley kutoka jimbo la magharibi la Oregon, alitangaza Jumapili kuunga mkono mkataba wa kimataifa wa kuizuia Iran kutengeneza silaha za nyuklia. Merkley amekuwa seneta wa 31 kusema kwamba atapiga kura mwezi ujao kuukubali mkataba huo na kumuongezea Rais Barack Obama hesabu za kukaribia kuona kwamba mkataba huo utaendelea kama ulivyo.

Mkataba huo uliosimamiwa na Marekani na mataifa matano yenye nguvu duniani unataka ufuatiliaji wa kimataifa wa program ya nyuklia ya Tehran huku vikwazo vya Umoja wa Mataifa na magharibi ambavyo vimezorotesha uchumi wa Iran vitaondolewa.

Jengo la bunge la Marekani
Jengo la bunge la Marekani

Bunge na baraza la seneti la Marekani ambayo yote yanadhibitiwa na wapinzani wa bwana Obama wa Republican wanapanga kuupigia kura mkataba huo kati kati ya mwezi Septemba. Hakuna m-Republican yeyote anayezungumza kuunga mkono mkataba huo na wachambuzi wanatabiri baraza la wawakilishi litapiga kura ya kuukataa mpango huo.

Katika baraza la seneti hata hivyo kura inakaribia kukiwa na wanachama 54 wengi wa Republican wakihitaji wa-Democrat sita kupinga mkataba huo ili kuweza kupata idadi ya kura 60 zinazohitajika katika baraza la seneti lenye wanachama 100 kuweza kuukataa mkataba huo. Hadi sasa ni wa-Democrat wawili pekee ndio wametangaza kuupinga kwao mkataba huo.

Kote baraza la seneti na bunge wanakataa mkataba huo ambapo bwana Obama alisema atatumia kura ya turufu akiyalazimisha mabaraza yote mawili kupata theluthi mbili kuweza kupinga kura yake ya turufu.

Seneta Jeff Merkley
Seneta Jeff Merkley

Katika baraza la seneti kura 34 zitatosha kwa rais kutumia kura ya turufu na kwa uungaji mkono wa Merkley, bwana Obama hivi sasa yupo kura tatu mbele kutoka kura zinazohitajika. Wafuasi wa Democrat wa bwana Obama katika seneti wanajaribu kupata uungaji mkono zaidi kwa mkataba huo kutoka angalau maseneta 41 ambao wataondoa haja ya rais kutumia kura ya turufu kama mkataba utapata upinzani.

Merkley alisema anafikiri mkataba una masuala muhimu yanayotarajiwa kujitokeza lakini hiyo ni njia bora ya kuizuia Iran kutotengeneza silaha za nyuklia.

XS
SM
MD
LG