Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 01, 2024 Local time: 23:23

Mkataba wa kihistoria umefikiwa juu ya mpango wa nuklia wa Iran

Viongozi walohusika mkatika majadiliano ya mpango wa nuklia wa Iran wakipiga picha pamoja, Julai 14, 2015.
Viongozi walohusika mkatika majadiliano ya mpango wa nuklia wa Iran wakipiga picha pamoja, Julai 14, 2015.

Mataifa makuu ya dunia yamefikia makubaliano ya kihistoria na Iran juu ya mpango wa nuklia wa Teheran mjini Vienna Austria. Mkataba huo utapunguza uwezo wa Iran kutengeneza silaha za nuklia ili nayo iweze kuondolewa kwa awamu vikwazo vya kiuchumi.

Mkuu wa masuala ya kigeni wa EU Federica Mogherini na waziri wa mambo ya kigeni wa Iran Mohammad Javad Zarif wakitangaza mkataba wa kihistoria Vienna, Austria, July 14, 2015.
Mkuu wa masuala ya kigeni wa EU Federica Mogherini na waziri wa mambo ya kigeni wa Iran Mohammad Javad Zarif wakitangaza mkataba wa kihistoria Vienna, Austria, July 14, 2015.

Mkuu wa masuala ya kigeni wa Jumuia ya Ulaya Federica Mogherini na waziri wa mambo ya nchi za nje wa Iran Javad Zarif walitangaza mkataba huo mjini Vienna kufuatia wiki kadhaa ya mazungumzo marefu juu ya kukamilisha kila kipengele cha mkataba huo.

Rais Barack Obama, akisimama na Makamu Rais Joe Biden, akizungumzia mkataba na Iran
Rais Barack Obama, akisimama na Makamu Rais Joe Biden, akizungumzia mkataba na Iran

Rais Barack Obama akizungumza mara baada ya kutangazwa mkataba huo amesema"mkataba huu unadhihirisha kwamba diplomasia ya Marekani inaweza kupelekea kupatikana mabadiliko ya kwerli na ya maana."

Rais alisema atatumia kura yake ya turufu kupinga sheria yeyote katika bunge la Marekani ambayo itajaribu kuzuia mkataba huo. "Mkataba unatowa fursa ya kusonga mbele kwa njia mpya." aliongeza kusema Obama.

Kwa mara ya kwanza katika kitendo cha Nadra hotuba ya kiongozi wa Marekani ilitangazwa moja kwa moja na vituo vyote vya televisheni nchini Iran.

Na mara baada ya hotuba ya Obama hapa Washington, Rais wa Iran Hassan Rouhani alipongeza makubaliano hayo na kusema "ukurasa mpya" umeanza katika uhusiano na dunia.

Waziri wa mambo ya nje wa marekani John Kerry akizungumzia mkataba wa nuklia
Waziri wa mambo ya nje wa marekani John Kerry akizungumzia mkataba wa nuklia

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani John Kerry, akizungumza mjini Vienna Jumanne, alikaribisha mkataba lakini alionya kwamba "ikiwa Iran itashindwa kwa njia yeyote kuheshimu' ahadi zake basi vikwazo vitarudishwa mara moja.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:48 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

XS
SM
MD
LG