Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 08:01

Marekani : Zuckerberg akutana na Trump, wakosoaji wake Bungeni


Mark Zuckerberg akiwasili katika Bunge la Marekani kukutana na wabunge
Mark Zuckerberg akiwasili katika Bunge la Marekani kukutana na wabunge

Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Facebook Mark Zuckerberg amekutana na Rais Donald Trump pamoja na wabunge kadhaa ambao wamekuwa wakikosoa mwenendo wa biashara yake.

Alhamisi jioni, Trump alituma ujumbe wa Tweeter “mkutano mzuri” na kuposti picha wakiwa katika ofisi ya Oval, White House. [[https://twitter.com/realDonaldTrump/status/1174836342552969217 ]]

Msemaji mmoja wa Facebook alisema muasisi wa Facebook alikuwa mjini Washington Alhamisi kukutana na wabunge “kusikiliza dukuduku waliokuwa nalo na kuongelea juu ya mustakbali wa usimamizi wa intaneti.

Zuckerberg alisikia mambo mengi zaidi kuliko malalamiko kutoka kwa wakosoaji wake wakuu katika Bunge la Marekani, kati yao akiwemo Seneta Josh Hawley, Mrepublikan kutoka Missouri.

Haley alisema alimwambia Zuckerberg “kuthibitisha” kuwa alikuwa anania thabiti ya kulinda usiri wa takwimu na kuwepo ushindani. “Alimpa changamoto za kufanya mambo mawili kuonyesha kuwa FB inania thabiti juu ya kukabiliana na ukandamizaji wa maoni mbadala, kulinda faragha ya wateja na kuwepo ushindani. 1) Ziuze WhatsApp na Instagram 2) Wasilisha maudhui kwa taasisi inayojitegemea, uhakiki ufanywe juu ya udhibiti wa yanayotumwa katika mitandao na taasisi nyingine. Alikataa mambo yote mawili,” Hawley alituma ujumbe wa tweet baada ya mkutano. [[ https://twitter.com/HawleyMO/status/1174777452285038595 ]]

Zuckerberg pia alikutana na maseneta wengine, akiwemo Mdemokrat Mark Warner wa Virginia na Mrepublikan Mike Lee wa Utah. Pamoja na kufuatwa na waandishi wa habari, alikataa kujibu maswali yoyote juu ya mikutano aliyoifanya.

Ziara ya Zuckerberg ilikuwa na lengo la kubadilisha mazungumzo yanayoendelea Bungeni juu ya hatua ya kuandaa sheria ya kulinda takwimu ambayo itaruhusu wateja wa makampuni ya teknolojia kama Facebook, Google, Amazon na Apple kuweka katazo la kutumia takwimu walizokuwa nazo.

XS
SM
MD
LG