Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 05:16

Marekani yaomboleza vifo vya waliouawa katika shambulizi la bunduki Texas


Texas: Wabunge wa Marekani waeleza nini kifanyike kukabiliana na mauaji nchini
please wait

No media source currently available

0:00 0:02:39 0:00

Texas: Wabunge wa Marekani waeleza nini kifanyike kukabiliana na mauaji nchini

Marekani inaomboleza vifo vya watoto 19 na watu wazima watatu ambao waliuawa huko Uvalde, Texas, macho yameanza kugeuzwa kuiangalia Washington kuona hatua gani zitachukuliwa – kama kuna zozote, ikiwa wabunge watachukua hatua kuhusu sheria ya umiliki wa bunduki. 

Capitol Hill inaoenkana ina harakati za wabunge wakiangalia jinsi ya kuchukua hatua.

Seneta Chris Murphy wa Connecticut alisema kwamba alizungumza na mwenzake mdemocrat, Joe Manchin, na waote walipanga kuzungumza na warepublican kuhusu kupendekeza uwezekano wa uchunguzi wa kina na mapungufu yaliyopo katika sheria.

Afisa polisi alisema waathirika wote walikuwa ni wanafunzi wa darasa la nne, kwa mujibu wa shirika la habari la Associated Press, akizungumza katika mahojiano na kituo cha televisheni cha CNN na afisa wa idara ya usalama ya Texas, Luteni Christopher Olivarez.

Rais Joe Biden alitoa hotuba yenye hisia kali akitaka kuwepo kwa masharti mapya kuhusu umiliki wa silaha.

Rais Joe Biden
Rais Joe Biden

Rais Joe Biden ameeleza haya: "Wamarekani wengi wanauunga mkono sheria za kawaida zenye kuleta maana, sheria za bunduki. Nimetoka tu hivi punde kwenye ziara ya Asia na kukutana na viongozi wa Asia. Nimepata habari hizi nikiwa ndani ya ndege. Kilichonishtua katika safari ya saa 17. Kilichonishtua ni aina hii ya mauaji ya watu wengi kuhusu bunduki ni nadra sana kutokea kwingineko duniani. Kwanini? Wana matatizo ya akili. Wana mizozo ya ndani katika nchi nyingine. Wana watu aboa wamepotea. Lakini aina hii ya mauaji ya ufyatuaji risasi kamwe hayatokea mara kwa mara kama ilivyo Marekani. Kwanini?”

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson Jumatano alituma salama za rambi rambi kwa jamaa wa waathirika

Waziri Mkuu Boris Johnson
Waziri Mkuu Boris Johnson

Johnson alisema: "Bwana spika, nataka kuanza kwa kuunga mkono ulichosema kuhusu ripoti mbaya sana za ufyatuaji risasi huko Texas katika shule moja ya msingi. Mawazo yetu yako kwa wote wale ambao wameathiriwa na shambulizi hili baya sana.”

Papa Francis Jumatano alisema “amesikitishwa sana na mauaji hayo.”

Papa Francis amesema haya: "NImesikitishwa sana na mauaji kwenye shule ya msingi huko Texas. Nawaombea watoto na watu wazima waliouawa na familia zao. Wakati umefika kwa kusema inatosha kwa umiliki holela wa silaha. Sote tuna nia ya dhati ili majanga kama haya yasitokee tena.”

Jana, kiongozi wa walio wengi katika baraza la senate Chuck Schumer alianza mchakato wa kuwasilisha miswaada miwili ambayo ilipitishwa na bunge, na kuiweka yote miwili katika kalenda ya Senate kwa uwezekano wa kupigiwa kura. Mswaada mmoja utaongeza kipindi cha uchunguzi kwa wanunuzi kutoka siku tatu mpaka kumi.

XS
SM
MD
LG