Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 10:03

Marekani yafunga njia zote zilizokuwa zinatumiwa na Russia kwa kulipa madeni yake


Jengo la wizara ya fedha ya Marekani. Picha ya AP
Jengo la wizara ya fedha ya Marekani. Picha ya AP

Marekani imesema itafunga njia ya mwisho kwa Russia kulipa mabilioni ya dola ya deni lake kwa wawekezaji wa kimataifa leo Jumatano, na kufanya Russia kushindwa kulipa madeni yake kwa mara ya kwanza tangu wakati wa mapinduzi yajulikanayo kama ya Bolshevik ya mwaka wa 1917.

Wizara ya fedha ya Marekani imesema katika taarifa kwamba haina mpango wa kutoa leseni mpya ili kuiruhusu Russia kuendelea kuwalipa wakopeshaji wake kupitia benki za Marekani.

Tangu awamu ya kwanza ya vikwazo, wizara ya fedha ya Marekani ilizipa benki leseni ya kushughulikia malipo yoyote ya dhamana kutoka Russia. Muda wa fursa hiyo unakamilika saa sita usiku Mei 25.

Kumekuwa pia ishara kwamba utawala wa Biden hauna niya ya kuongeza muda huo wa kikomo.

Bila leseni ya kutumia benki za Marekani kulipa madeni yake, Russia haitakuwa na uwezo wa kulipa dhamana za wawekezaji wake wa kimataifa.

Kremlin imekuwa ikitumia Benki ya JPMorgan Chase na Citigroup kama njia ya kulipa madeni yake.

XS
SM
MD
LG