Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 19:59

Marekani yamwekea vikwazo mkuu wa jeshi la polisi DRC


Rais wa drc Joseph Kabila katikati kwenye picha
Rais wa drc Joseph Kabila katikati kwenye picha

Marekani imemuwekea vikwazo mkuu wa jeshi la polisi nchini Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo katika mji wa Kinshasa kutokana na ghasia na mauaji ya raia.

Mali zote zilizoko Marekani za Celestin Kanyama zimezuiwa na Marekani imempiga marufuku kufanya biashara yoyote na nchi yake.

Marekani inamshutumu Kanyama na jeshi la polisi kwa kutengeneza mazingira ya hofu nchini Drc kabla ya uchaguzi mkuu unatorajiwa kufanyika desemba mwaka huu.

Rais Joseph Kabila anatarajiwa kufanya marekebisho ya sheria ya uchaguzi ili kumruhusu yeye kugombea kwa muhula wa tatu ambao utakiuka katiba.

Utawala wa rais Obama umesema Kenyama anaongoza jeshi la polisi kutumia ghasia ili kuzuiya wapinzani wa kabila ikiwemo mashambulizi kwa wanawake na watoto na kusababisha takriban vifo vya watu 40. Polisi ilivamia nyumba kadhaa katika mji wa Kinshasa na kuwaburuza watuhumiwa wa upinzani wakiwa wamewanyooshea bunduki bila kuwa na kibali cha kuwakamata.

Takriban vijana 50 na wavulana waliuwawa na wengine 30 hawajulikani walipo.

Afisa wa hazina wa marekani Jonh Smith anasema vikwazo hivyo vinatuma ujumbe ulio wazi kwamba Marekani inalaani utawala, ghasia na hatua za ukandamizaji hasa zile za Celestin Kanyama ambazo zinatishia demokrasia ya mbeleni kwa watu wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

XS
SM
MD
LG