Barbara Bush, mke wa Rais mstaafu wa Marekani George H.W. Bush alifariki Aprili 17, 2018 akiwa na umri wa miaka 92.
Marehemu Barbara atazikwa katika eneo la Maktaba ya Bush huko chuo kikuu cha Texas A&M kilichopo kilomita 160 kutoka Houston, ambapo mtoto wao Robin aliyekufa akiwa na miaka mitatu amezikwa.