Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Februari 08, 2025 Local time: 18:48

Mapigano makali yazuka Ethiopia katika mji wa kihistoria


Waumini wakiwa katika ibada huko Lalibela, mji wa kihistoria wa Ethiopia Januari 27, 2022. Picha na REUTERS/Tiksa Negeri
Waumini wakiwa katika ibada huko Lalibela, mji wa kihistoria wa Ethiopia Januari 27, 2022. Picha na REUTERS/Tiksa Negeri

Mapigano makali yalizuka Jumatano katika mji wa kihistoria wa Lalibela nchini Ethiopia kati ya vikosi vya serikali na kundi la wanamgambo wa eneo hilo, wakaazi wa eneo hilo walisema.

Si mara ya kwanza kwa eneo hilo la Urithi wa Dunia la UNESCO kukumbwa na mapigano katika mkoa wa Amhara kati ya Jeshi la Taifa la Ulinzi la Ethiopia na kundi lenye silaha linalojulikana kama Fano.

"Mapigano yalianza asubuhi ya leo majira ya saa mbili, bado tunasikia mapigano ya risasi. Inaonekana Fano wanadhibiti sehemu za mji. Naweza kuona vikundi vidogo kwenye barabara kuu," dikon wa kanisa la Lalibela aliliambia shirika la habari la AFP, kwa masharti ya kutotajwa jina lake kwa sababu za kiusalama.

Wawakilishi wa serikali ya shirikisho au msemaji wa vikosi vya jeshi hawakuweza kupatikana kutoa maoni au hawakujibu mara moja ujumbe uliotumwa kutoka shirika la habari la AFP. "

Jana usiku Fano ilikaribia Lalibela kutoka pande nne na mapigano yalianza leo asubuhi majira ya saa mbili," mkazi mwingine aliliambia shirika la habari la AFP.

Ni vigumu kwa AFP kuthibitisha kutoka vyanzo huru hali ilivyo katika eneo la Amhara, kwasababu fursa kwa vyombo vya habari kwenda katika mkoa huo imewekewa masharti makali.

Chanzo cha habari hii ni shiika la habari la AFP

Forum

XS
SM
MD
LG