Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Februari 09, 2025 Local time: 08:41

Dunia yadaiwa kufumbia macho mgogoro wa Sudan


FILE PHOTO: Fleeing Sudanese seek refuge in Chad
FILE PHOTO: Fleeing Sudanese seek refuge in Chad

Afisa mwandamizi wa shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa Jumanne alionya kwamba "mgogoro wa kibinadamu uliopindukia" unaendelea nchini Sudan, huku mamilioni ya watu wakilazimika kuyahama makazi yao kutokana na mzozo unaozidi kuwa mbaya.

"Nilichokiona kinakatisha tamaa, mahitaji makubwa ya kibinadamu ni makubwa kupindukia na hofu imetanda machoni mwa watu wengi," Dominique Hyde, Mkurugenzi wa Mahusiano ya Nje wa UNHCR alisema. "Hivi ni vita vilivyozuka ghafla na vimeigeuza Sudan iliyokuwa nchi ya amani kuwa makaburi."

Hyde amerejea kutoka katika ziara ya wiki moja katika Jimbo la White Nile nchini Sudan pamoja na kwenda mpakani na maeneo mengine ya Sudan Kusini.

Alisema ukatili na mapigano yanaongezeka kupita kiasi wakati ulimwengu ukibaki " na kashfa ya ukimya, ingawa ukiukwaji wa sheria za kimataifa za binadamu unaendelea bila ya khofu ya kuchukuliwa hatua."

Tangu mapigano yalipozuka Aprili 15 kati ya Vikosi vya jeshi la Sudan na Vikosi vya Msaada wa Dharura vya Wanajeshi, UNHCR inaripoti kuwa watu milioni 4.5 wameyakimbia makazi yao ndani ya Sudan, wakati watu milioni 1.2 wamekimbilia nchi jirani, zikiwemo Chad, Misri, Sudan Kusini, Ethiopia na Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Mapigano ya hivi karibuni katika jimbo la Darfur nchini Sudan yamesababisha watu wengi zaidi kuyahama makazi yao, huku maelfu ya watu wakihangaika kutafuta makazi na wengi wao kulala chini ya miti kando ya barabara, alisema Hyde, akiongeza kuwa wengi wa wakimbizi hao ni wanawake na watoto.

Forum

XS
SM
MD
LG