“Hakuna suluhisho lililokubalika la kijeshi kwa mzozo huu,” amesema msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani, Mathew Miller. “Tunawataka SAF na RSF kuchukua mwelekeo wa mazungumzo yenye tija, kwa lengo kuu la kuokoa maisha ya watu, kupungua mapigano na kuandaa njia ya mwelekeo wa mashauriano ili kuondoka katika vita,” ameongeza kusema Miller.
Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema Jumapili kwamba Marekani, Saudi Arabia Jumuiya ya IGAD, na Umoja wa Afrika wameanza tena juhudi za kibinadamu na mazungumzo ya sitisho la mapigano kati ya jeshi la Sudan na kikosi cha dharura cha Rapid Support Forces, RSF.
Forum