Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Februari 07, 2023 Local time: 15:30

Mamlaka ya San Francisco yafunguliwa mashtaka na watu wasiokuwa na makazi


Watu wasiokuwa na makazi wakiwa katika mitaa ya mji wa San Francisco.

Uongozi wa mji wa San Francisco, Marekani umeshtakiwa  kutokana na hatua ya kuwalazimisha watu wasio na makazi kuondoka na mali zao bila kuwapa makazi mbadala.

Takriban watu 7,800 wasio na makazi kwenye mji huo wenye siasa huru wamekuwa tatizo kwenye jimbo la California, wengi wao wakiishi kwenye mahema na magari.

watu wasiokuwa na makazi wakiishi karibu na takataka.
watu wasiokuwa na makazi wakiishi karibu na takataka.

Wamiliki wa nyumba, biashara pamoja na viongozi wanasema kwamba watu hao wanahatarisha afya pamoja na kuathiri matumizi ya maeneo ya umma kwa wakazi wengine.

Tatizo hilo pia linashuhudiwa kwenye majimbo kadhaa ya magharibi mwa Marekani wakati wanaharakati wa haki za wasio na makazi wakiwasilisha malalamiko kwenye mahakama.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG