Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 11:25

Jaji aamuru mshambuliaji wa Pelosi azuiliwe bila dhamana

David Wayne DePape ambaye anashtakiwa kwa kuvunja nyumba ya Spika wa Bunge la Marekani Nancy Pelosi na kumpiga mume wake kichwani kwa nyundo, ameketi karibu na wakili wake na mwendesha mashtaka mbele ya Jaji katika Mahakama ya Jinai mjini San Francisco, California Novemba 2022

Jaji wa San Francisco ameamuru mwanamume anayeshtakiwa kwa kuvunja nyumba ya Spika wa Bunge Nancy Pelosi, kumpiga mumewe na kutaka kumteka nyara, azuiliwe bila dhamana.

Adam Lipson, mtetezi wa umma aliyeteuliwa kumwakilisha David DePape, aliingia katika kesi ya wakili wa utetezi wa umma alisema mteja wake hana hatia wakati wa kusikilizwa kwa muda mfupi Jumanne katika Mahakama ya Juu huko San Francisco.

Ilikuwa ni mara ya kwanza kuonekana hadharani tangu shambulio la Ijumaa mapema la DePape, mwanaharakati wa mrengo wa kulia aliyevutiwa na nadharia za Mafumbo. Waendesha mashtaka wanadai kuwa alitaka kumteka nyara Spika Pelosi na kumvunja magoti yake kama onyo kwa wabunge wengine wa demokrat. Shambulio hilo dhidi ya Paul Pelosi mwenye umri wa miaka 82 lilileta mshtuko katika ulimwengu wa kisiasa siku chache kabla ya uchaguzi wa katikati ya muhula nchini Marekani.

XS
SM
MD
LG