Kesi hiyo imekuja muda mfupi baada ya mahakama ya kijeshi kutupilia mbali kesi ya kumiliki bunduki na risasi na kumwachia huru. Wananchi wa nchi jirani ya Kenya wamefanya maandamano kushinikiza serikali ya Uganda kumwachia huru msanii na mwanasiasa huyo. Haya ni baadhi ya matukio yaliyojiri katika maandamano nchini Kenya.
Mambo yaliyojiri baada ya Bobi Wine kushikiliwa na vyombo vya usalama Uganda
Mbunge wa Kyadondo Robert Kyagulanyi amefunguliwa mashtaka upya Alhamisi na serikali ya Rais Yoweri Museveni nchini Uganda kwa kutuhumiwa kuhusika na vitendo vya uhaini.

1
Wakenya wafanya maandamano ya kupinga kushikiliwa kwa Robert Kyagulanyi- Bobi Wine katika jela ya kijeshi nchini Uganda

2
Wakenya wakiandamana mjini Nairobi.

3
Wakenya wakionyesha mshikamano na wananchi wa Uganda kupinga kushikiliwa kwa Robert Kyagulanyi- Bobi Wine.

4
Wakenya wafanya maandamano ya kupinga kuwekwa kizuizini kwa Robert Kyagulanyi- Bobi Wine