Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 29, 2022 Local time: 06:44

Mama wa Kamanda wa Polisi aliyeuwawa Uganda asimulia


Muhammad Kirumira

Siku ya mwisho ya uhai wake Kamanda wa Wilaya ya Buyende, Muhammad Kirumira ambaye aliuwawa Jumamosi na watu wanaodaiwa kuwa walitumia bunduki kufanya mauaji hayo.

Gazeti la The Monitor limeripoti kuwa siku hiyo kabla ya kuuwawa Muhammad Kirumira ilikuwa zaidi ya kawaida kwa matukio mawili aliyohudhuria kabla ya tukio hilo, anasema mama yake Sarah Namuddu.

“Niliwasiliana naye Jumamosi saa tano asubuhi na tukaenda pamoja katika shughuli huko kitongoji cha Katereke, Nsangi,” Namuddu alieleza Jumapili.

Mama mzazi azungumza

“Aliniambia ana shughuli nyingine itakayo fanyika barabara ya Mityana. Aliniacha katika shughuli hiyo saa nane mchana na kwenda katika shughuli nyingine iliyokuwa ikifanyika barabara ya Mityana,” Namuddu anaeleza.

Namuddu anasema kuwa, Kirumira alikuwa mtoto wake wa tatu kati ya watoto sita.

Anasema kilicho mshitua ni taarifa kutoka kwa mwendesha bodaboda aliyemchukua katika piki piki kutoka kituo cha Busega roundabout.

“Ilikuwa majira ya saa mbili usiku. Mwenye boda boda hakujua mimi ni nani na akaniambia habari juu ya mtu mmoja anayeitwa Kirumira alivyokuwa amepigwa risasi. Aliniambia kuwa Kirumira alikuwa bado hai, lakini mimi nilisisitiza kuwa watu wanapopigwa risasi hawawezi kusalimika,” amesema.

Kirumira

Kirumira alikuwa katika gari aliporushiwa risasi karibu na nyumbani kwake huko Bulenga, Wilaya ya Wakiso. Washambuliaji hao walikuwa wamepanda bodaboda.

Masaa kadhaa kabla ya kuuwawa karibu na nyumbani kwake alikuwa ametuma ujumbe wa kuwapongeza waandishi wa habari nchini Uganda ambao walikuwa wamemaliza kuchagua viongozi wao.

Ibrahim Abiriga

Miezi miwili iliyopita, Mbunge wa zamani wa Manispaa ya Arua Ibrahim Abiriga akiwa ndani ya gari na kaka yake Saidi Kongo walipigwa risasi katika tukio linalofanana na hili la Kirumira.

Andrew Felix Kaweesi

Mwezi Machi mwaka 2017, Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi Andrew Felix Kaweesi aliuwawa na watu wenye bunduki mara tu alipokuwa akiondoka nyumbani kwake huko Kulambiro karibu na Kampala. Pia mlinzi wake Kenneth Erau na dereva wake Godfrey Mambewa waliuwawa.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG