Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 07, 2024 Local time: 11:24

Arua yapokea mwili wa mbunge wao kwa huzuni kubwa


Marehemu Ibrahim Abiriga
Marehemu Ibrahim Abiriga

Shughuli zote za biashara zilisimama katika mji wa Arua nchini Uganda Jumapili mchana baada ya mwili wa Mbunge Ibrahim Abiriga na ndugu yake, Buga Said waliouwawa kwa kupigwa risasi kuwasili uwanja wa ndege.

Muda mfupi baada ya kuwasili, helikopta ilionekana ikiruka juu angani ikizunguka ikitoa ishara kwa wananchi kuwa mwili wa mbunge huyo ulikuwa umekwisha wasili.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor mamia ya waombolezaji walifunga maduka yao kusubiri miili ya marehemu hao kabla ya kuandamana.

Mara tu baada ya ndege hiyo kutua majira ya saa kumi na dakika arubaini jioni, wananchi walivamia kiwanja cha ndege, bila kujali katazo la kuvuka kuingia uwanjani.

Waombolezaji kadhaa walijiangusha chini wakilia kwa kuonyesha huzuni yao kwa kumpoteza mbunge wao mpendwa.

XS
SM
MD
LG