Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 01:45

Makamanda wa kijeshi wakutana Nairobi, viongozi wa EAC kukutana Jumatatu


Wanajeshi wa serikali ya DRC
Wanajeshi wa serikali ya DRC

Makamanda wa kijeshi wa nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki walikutana mjini Nairobi Jumapili kukamilisha maandalizi ya kutumwa kwa kikosi cha pamoja Mashariki mwa DRC, katika juhudi za kutafuta amani huku serikali ya Kenya ikitangaza kwamba mkutano wa viongozi wa EAC utafanyika Jumatatu.

Viongozi wa mataifa wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki watakutana Jumatatu kujadili hali ya usalama katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Afisi ya rais wa Kenya ilimesema Jumapili.

Mkutano huo unajiri wakati mapigano makali yamefufua uhasama wa miongo kadhaa kati ya Kinshasa na Kigali, huku DRC ikiilaumu jirani yake, Rwanda, kwa kuibuka upya hivi karibuni kwa kundi la waasi la M23. Rwanda imekanusha mara kwa mara kuwaunga mkono waasi hao huku nchi zote mbili zikilaumiana kwa kufanya mashambulizi ya kuvuka mpaka.

“Watu mashariki mwa DRC wameteseka kwa muda mrefu na wanaendelea kulipa gharama kubwa kupita kiasi kwa kupoteza maisha, mali na ukosefu wa amani," afisi ya rais wa Kenya ilisema katika taarifa yake ya kutangaza mkutano wa Jumatatu mjini Nairobi. Siku ya Jumatano, Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alitoa wito wa kutumwa kwa kikosi cha kanda ya Africa mashariki nchini DRC ili kurejesha hali ya amani, lakini Kinshasa ilisema haitakubali ushiriki wa Rwanda katika operesheni hiyo.

Rais wa DRC Felix Tshisekedi ameishutumu Rwanda kwa kutaka "kuchukua ardhi yetu, yenye utajiri wa dhahabu, kobalti na madini mengine, kwa ajili ya kujinufaisha" na kuitaka jumuiya ya kimataifa kulaani Kigali.

Kikosi cha Umoja wa Mataifa kinachojulikana kwa kifupi kama MONUSCO, tayari kipo nchini DRC.

XS
SM
MD
LG