Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 24, 2024 Local time: 03:04

DRC yaitaka Rwanda kutoshiriki katika kikosi cha pamoja cha kikanda


Rais wa Rwanda Paul Kagame
Rais wa Rwanda Paul Kagame

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inataka Rwanda izuiliwe kushiriki katika kuundwa kwa kikosi cha kijeshi, cha kikanda, kilichopendekezwa, katika juhudi za kuimarisha usalama nchini humo.

Serikali ya Rais Felix Tshisekedi inaiomba Uingereza kuishinikiza Kigali kukomesha kile ilichokiita "uchokozi" wake, Kinshasa imesema.

Huu ni mzozo wa hivi punde kati ya majirani hao wawili, ambao wana historia ya miongo kadhaa ya malumbano, na hivi karibuni kumeshuhudiwa mapigano ya hapa na pale kwenye mpaka wao wa pamoja.

Kinshasa ilidai katika taarifa yake kwamba "magaidi" wa kundi la waasi la M23, ambao ilisema wanaungwa mkono na Rwanda, siku ya Jumatatu waliuteka na kupora mji wa Bunagana, ulio kwenye mpaka wa DRC na Uganda.

Hapo awali serikali ililaani kile ilichokiita "ukiukaji wa makusudi wa uadilifu wa eneo" la DRC. Taarifa hiyo ilisema kuwa Rais Felix Tshisekedi aliongoza kikao kisicho cha kawaida, cha baraza kuu la ulinzi siku ya Jumatano, ambapo DRC ilichukua hatua ya kusitisha makubaliano ya kidiplomasia na Rwanda.

Tshisekedi alitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa, hususan Marekani na Uingereza, "kulaani uvamizi huo, na kuishinikiza Rwanda kuondoa wanajeshi wake katika ardhi ya DRC."

XS
SM
MD
LG