Imesema uchunguzi unaonyesha kwamba mizoga ya vifaru weusi kaskazini mwa hifadhi ya wanyama ya Etosha walikuwa kati ya umri wa wiki tatu na wazee.
Taarifa zinasema hii inaonyesha kuwa mapambano dhidi ya uwindaji haramu bado hayajamalizika.
Hakuna mtu yeyote aliyekamatwa kuhusiana na tukio hili, wakati ambapo uchunguzi bado unaendelea.
Wizara imeomba raia yeyote wa Namibia mwenye maelezo kutoa taarifa katika kituo cha polisi au kwenye wizara hiyo.
Jumla ya vifaru 22 wameuwawa na wawindaji haramu tangu mwanzoni mwa mwaka huu, kwa mujibu wa wizara hiyo.