Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 23, 2024 Local time: 08:13

Namibia yapiga marufuku uagizaji wa ndege kutokana na mlipuko wa homa ya ndege


Serikali ya Namibia imepiga marufuku uagizaji wa ndege wa kufuga na bidhaa zitokanazo na ndege hao kutoka Ujerumani na Uholanzi kutokana na mlipuko wa mafua ya ndege katika nchi za ulaya.

Ujerumani iliripoti mlipuko wa homa ya ndege wiki iliyopita huku mashamba ya kufuga ndege kote Uholanzi yakiamrishwa kutowaachilia huru ndege wote baada ya kisa cha maambukizi ya homa ya ndege kuripotiwa katika mkoa wa Flevoland.

Idara ya tiba kwa mifugo nchini Namibia imesema kwamba imesitisha uagizaji wa ndege na bidhaa zote za ndege kuingia nchini humo kutoka nchi hizo mbili.

Imesema kwamba ndege waliokuwa wameshapakiwa tayari kupakiwa kuanzia Oktoba 1 nchini Ujerumani, na Oktoba 5 nchini Uholanzi, hawataruhusiwa kuingia nchini humo, na kwamba watachomwa moto watakapowasili, huku muagizaji akigharamia shughuli hiyo.

Hatari ya binadamu kuambukizana homa ya ndege ni ndogo sana.

Mlipuko wa awali wa homa ya ndege ulipelekea idadi kubwa ya ndege kuchinjwa ili kudhibithi maambukizi.

XS
SM
MD
LG