Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 19:01

Al-Shabab 7 wahukumiwa kifo na Mahakama ya kijeshi Somalia


Bomu lililoripuka karibu na mgahawa huko Mogadishu, Somalia, kufuatia shambulizi la al-Shabab
Bomu lililoripuka karibu na mgahawa huko Mogadishu, Somalia, kufuatia shambulizi la al-Shabab

Watu saba wanaodaiwa kuwa ni wapiganaji wa al-Shabab wamehukumiwa adhabu ya kifo kwa kupigwa risasi katika mkoa wa Puntland kaskazini mashariki ya Somalia Ijumaa, Maafisa wametoa taarifa.

Mwendesha mashtaka wa mahakama ya kijeshi ya Puntland Abdullahi Hersi Elmi amesoma hukumu hiyo akisema kuwa watu wote saba wamekutwa na makosa kuwa kuhusika na mauaji na tuhuma nyingine za ugaidi. Amesema angalau mtu mmoja kati yao amekubali makosa hayo.

Watu watano walikamatwa katika kizuizi karibu na Bosaso Aprili wakati wakijaribu kuvusha mabomu ndani ya mji huo, maafisa hao wamesema.

Watu hao ni vijana wenye umri kati ya miaka 20 mpaka 22, mmoja ni miaka 26 na watano aliyehukumiwa ni miaka 27.

“Walikamatwa karibu na Bosaso wamebeba magunia 5 ya mabomu katika gari,” Elmi ameiambia mahakama. Hersi hakusema iwapo kulikuwa na mashtaka yoyote ya mauaji dhidi ya watuhumiwa hao.

Mahakama hiyo imesema kuwa watuhumiwa wawili ambao waliuawa leo walikamatwa huko Galkayo mwaka 2015 na walikuwa tayari wamehukumiwa kifo. Elmi amedai kuwa mmoja kati yao alikiri kuwa amehusika katika mauaji ya watu 23 wakiwemo maafisa wa mkoa.

Puntland siku za nyuma ilikuwa imetuhumiwa kuwauwa baadhi ya washukiwa waliokuwa chini ya umri wanaopaswa kuingizwa hatiani. Shirika la Haki za Binadamu Amnesty International limesema watu wanne waliouawa Aprili walikuwa kati ya miaka 14 na 17. Wakati huo Amnesty International ikiwasihi Puntland kusitisha kupitisha hukumu hiyo ya kifo kwa watoto hao wawili waliohukumiwa na mahakama hiyo kwa madai ya kushiriki katika mauaji ya maafisa wa ngazi ya juu.

Amnesty imesema kuwa watoto hao kati ya miaka 17 na 15 walipaswa kushtakiwa katika mahakama ya watoto “bila ya kuwepo chaguo la adhabu ya kifo,” Lakini hatima yao haijulikani.

Wakati huohuo bomu limeripuka na kuua afisa wa jeshi la Somalia na kumjeruhi mwengine katika eneo la kaskazini magharibi nje ya mji ya makao makuu, Mogadishu Ijumaa usiku.

Afisa mwenye cheo cha meja aliuawa na askari mwengine kujeruhiwa kufutia bomu la kutengenezwa kienyeji kutegwa katika gari lake ambalo liliripuka.


XS
SM
MD
LG