Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 28, 2022 Local time: 21:56

Mahakama ya ICC yamkuta Ntaganda na makosa ya jinai ya kivita


Bosco Ntaganda akiwa mahakamani

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) imemkuta na makosa yote 18 ya jinai ya kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu kiongozi muasi wa zamani wa Congo Bosco Ntaganda Jumatatu.

Ntaganda alikuwa amekanusha kuwa ni muuaji na mhalifu wa kivita alipozungumza katika kesi yake huko mjini The Hague Alhamisi.

Katika hotuba kwa majaji wa ICC, Ntaganda alikiri kuwa alisifika kama “Muuaji” lakini alisema, “Mimi siko hivyo.”

Ntaganda alisisitiza kuwa yeye ni askari, na siyo mhalifu. Alisema, “Sijawahi kuwashambulia raia… siku zote nimekuwa nikiwalinda.”

Maoni hayo yamelepa mpishano mkubwa kwa wasifu walioutoa waendesha mashtaka wa ICC, ambao wanasema Ntaganda aliongoza kikundi cha waasi, UPC, kilichouwa, kuwabaka na kuwanyanyasa watu upande wa jimbo la Ituri mashariki ya Congo mwaka 2002 na 2003.

Wakili wa waathirika hao ameiambia mahakama kuwa wasichana ambao wana miaka 12 walilazimishwa kutumikia kama wake za makamanda wa ngazi ya juu wa kikundi hicho cha waasi.

Makosa hayo 18 ya jinai ya kivita na uhaldifu dhidi ya ubinadamu, ni pamoja na tuhuma za mauaji, utumwa wa kingono, kuwalazimisha watoto kuwa askari na kuhamisha wananchi kwa nguvu kutoka katika maeneo yao.

Mashambulizi ya UPC yanadaiwa kulenga makundi ya kikabila maalum kama vile Lendu, Bira na Nande. Moja wa mshiriki mwenza wa jinai hiyo ni Thomas Lubanga, ambaye alihukumiwa miaka 14 kutumikia kifungo mwaka 2012 baada ya ICC kumkuta na makosa ya kuwalazimisha watoto kutumika kama askari.

Ntaganda alikuwa hajulikani haliko kwa miaka saba baada ya kukutikana na makosa mwaka 2006, akiwakasirisha maafisa wa mahakama kwa kule konekana kwake baadhi ya nyakati kama maeneo ya umma.

Nin muasisi wa kikundi cha waasi cha Congo M23 mwaka 2012. Katika hatua ya kushangaza, alijisalimisha ubalozi wa Marekani huko Kigali, Rwanda, Machi 2013. Wataalam wanasema inawezekana alifanya hivyo kwa sababu kushiriki kwake kupigana ndani ya kundi la M23 kulimfanya ahofie maisha yake.

Waendesha mashtaka waliwaita darzeni ya mashahidi dhidi yake, wakiwemo baadhi ya watoto waliokuwa walazimishwa kutumika kama askari.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG