Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 13:33

Mahakama yaamuru watoto waliotumikishwa DRC kulipwa fidia


Aliyekuwa mbabe wa Kivita Thomas Lubanga akiwa mbele ya mahakama ya ICC, Uholanzi Disemba 1, 2014.
Aliyekuwa mbabe wa Kivita Thomas Lubanga akiwa mbele ya mahakama ya ICC, Uholanzi Disemba 1, 2014.

Mahakama ya Kimataifa ya Jinai, ICC, Ijumaa imeamrisha kuwa watoto walioingizwa kutumikia kikundi cha Thomas Lubanga huko Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kulipwa fidia ya dola milioni 10.

Thomas Lubanga ambaye aliitikisa DRC kivita alihukumiwa kifungo cha miaka 14 kwa makosa ya kuwateka watoto wadogo ambao wengine walikuwa chini ya miaka 11.

Watoto hao walilazimishwa kupigana katika eneo la Ituri iliyoko Mashariki mwa DRC.

Mawakili watetezi wa watoto hao walijenga hoja na kudadisi maisha ya watoto hao yaliyopokonywa yanaweza kupewa thamani na kulipwa.

Baada ya watoto hao kukombolewa kutoka katika utekaji huo wengi wao wakiwepo wasichana wamekataliwa kuungana na jamii zao.

XS
SM
MD
LG