Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 10, 2024 Local time: 20:56

Spika wa Tanzania asema atamtembelea Tundu Lissu


Tundu Lissu
Tundu Lissu

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema kuwa amepanga kwenda kumtembelea Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, ambaye anaendelea na matibabu nchini Kenya.

Lissu anatibiwa katika hospitali ya Nairobi nchini Kenya, kufuatia kupigwa risasi Septemba 7, 2017 wakati wa vikao vya bunge katika mji mkuu wa Tanzania, Dodoma.

Lissu alikuwa amelalamika kuwa hakupata msaada wowote kutoka katika Bunge ambapo yeye siyo tu ni mbunge bali ni mnadhimu wa kambi ya upinzani Bungeni.

Job Ndugai amesema “tutakwenda kumuona Tundu Lissu kwani ni mbunge wetu na sisi tunampenda sana.”

Spika wa Bunge amesema chama cha upinzani CHADEMA na pamoja na ndugu wa Tundu Lissu wangeandika barua kuhusu mbunge huyo kulipiwa matibabu sababu utaratibu wa kumpeleka Nairobi haukuwa utaratibu wa kawaida

Ndugai amesema kuwa kipindi cha nyuma alishindwa kwenda Kenya kwa kuwa nchi hiyo ilikuwa kwenye uchaguzi na haikuwa na utulivu wa kisiasa, na hivi sasa hali imetulia na anatarajia kwenda baada ya Christmas kumjulia hali.

"Mimi kama Spika siwezi kwenda na kutoka navyotaka Kenya bali napokwenda kule lazima kuwe na taarifa rasmi za kiserikali na kibunge na ninapokelewa hivyo na ninapopelekwa huko hospitali au wapi napelekwa kwa utaratibu huo ndiyo utaratibu wa nchi kwa nchi. Haiwezekani wao wana mechi kama zile (Uchaguzi) halafu spika nazunguka zunguka Nairobi wanaweza kusema ajenda aliyokuja nayo huyu siyo hii, katika pande hizi mbili Watanzania wamemtuma huyu ana ajenda nyingine kwa hiyo unapokuwa kiongozi lazima ujiongeze" alisema Spika Ndugai

Baada ya Lissu kushambuliwa na watu wasiojulikana, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema kauli ya serikali ni ya kusikitisha juu ya madai kuwa Lissu alitakiwa kufanya maombi juu ya matibabu yake.

Mbowe alisema alidadisi ni maombi gani yaliyokuwa yanahitajika kuhusu mgonjwa kama Tundu Lissu aliyekuwa mahututi.

XS
SM
MD
LG