Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 19:13

Mahakama Rwanda yawaachia huru wapinzani wa Kagame


Diane Shima Rwigara, mkosoaji wa Rais Paul Kagame akiwasili mahakamani mjini Kigali Rwanda, Desemba 6, 2018.
Diane Shima Rwigara, mkosoaji wa Rais Paul Kagame akiwasili mahakamani mjini Kigali Rwanda, Desemba 6, 2018.

Mahakama Kuu mjini Kigali Alhamisi imemwachia huru kiongozi wa upinzani Diane Rwigara na mama yake Adeline Rwigara kwa kufuta mashtaka yanayowakabili ikiwemo kuchochea uasi na kughushi nyaraka.

Waendesha mashtaka walikuwa wanadai kuwa washtakiwa hao wawili wana hatia na kutaka wapewe adhabu ya kifungo cha miaka 22.

Muziki wa Gospel, machozi, vicheko na makofi yalitawala ndani ya mahakama ikiwa ni sehemu ya sherehe ya furaha ya kuachiwa kwao, baada ya Jaji Xavier Ndahayo kutangaza kuwa Diane Rwigara na mama yake Adeline Rwigara hawana hatiya.

Mahakama hiyo imesema kuwa ujumbe wa sauti wa akaunti za WhatsApp ambazo upande wa mashtaka ulitumia kufungua mashtaka ya uchochezi wa uasi dhidi yao hauwezi kueleza kwa ufasaha kitendo hicho cha uhalifu.

Mahakama hiyo pia imesema kuwa upande mashtaka haukuweza kuonyesha kuwa Diane Rwigara alikuwa ameshiriki kikamilifu katika madai ya kughushi kwa saini zilizo kuwa katika nyaraka zake za maombi ya kushiriki katika uchaguzi.

Hatimaye, mahakama ilitoa tamko kuwa wote wawili hawana makosa kwa mashtaka yote yanayowakabili.

Kwa upande wa familia ya Rwigara, matokeo haya yalikuwa yakustaajabisha.

Diane Rwigara aliwahakikishia wafuasi wake kuwa ataendelea na shughuli zake za kisiasa.

XS
SM
MD
LG