Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 08, 2023 Local time: 06:05

Mpinzani, mwanamuziki na wengine 2,140 waachiwa huru Rwanda


Victoire Ingabire Umuhoza akiwa nyumbani kwake Aprili 07, 2010, Kigali, Rwanda.
Victoire Ingabire Umuhoza akiwa nyumbani kwake Aprili 07, 2010, Kigali, Rwanda.

Rais Paul Kagame wa Rwanda ametoa msamaha kwa kiongozi wa upinzani Victoire Ingabire Umuhoza na mwanamuziki maarufu Kizito Mihigo.

Tamko la serikali lililotolewa Ijumaa jioni limeeleza “ Mkutano wa baraza la mawaziri ulioendeshwa na Rais Paul Kagame Jumamosi, umepitisha kuachiwa kwa wafungwa 2,140 waliokuwa wanastahiki msamaha huo chini ya vifungu husika vya sheria.

Kati ya hao waliopewa msamaha ni Kizito Mihigo na Victoire Ingabire Umuhoza, na wengine kati ya hao hukumu zao zilibadilishwa kwa uwezo aliopewa Rais kufuatia maombi yao ya hivi karibuni juu ya kupewa msamaha Juni 2018.

Kifungu cha 109 cha Katiba ya Rwanda kinasema : “Rais wa Jamhuri ya Rwanda ana uwezo wa kutumia mamlaka aliyopewa kutoa msamaha kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa na sheria na baada ya kushauriana na Mahakama ya Juu.

Mwaka 2013 Ingabire alihukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 15 na Mihigo alifungwa miaka 10 mwaka 2015.

XS
SM
MD
LG