Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 05, 2024 Local time: 15:39

Mahakama kuu ya Uholanzi yakata mtuhumiwa wa mauaji ya kimbari ya Rwanda kurudishwa Kigali


Nje ya kanisa la St. Pierre Kibuye, mjini Karongo, Rwanda ambako maelfu ya Watutsi waliuliwa wakati wa mauwaji ya kimbari ya Rwanda ya 1994.
Nje ya kanisa la St. Pierre Kibuye, mjini Karongo, Rwanda ambako maelfu ya Watutsi waliuliwa wakati wa mauwaji ya kimbari ya Rwanda ya 1994.

Mahakama Kuu ya Uholanzi siku ya Jumanne iliamua kwamba mtu anaekabiliwa na mashtaka ya mauwaji ya kimbari na uhalifu dhidi ya ubinadamu asirudishwe Rwanda kwa sababu hakuna uhakika kesi yake itakua ya haki.

Katika uwamuzi wake, Mahakama Kuu ilithibitisha uwamuzi ulotolewa na mahakama ya chini mwezi Novemba mwaka jana kwamba kurejeshwa nchini Rwanda kwa Pierre-Claver Karangwa kutakua na hatari "ya kukiuka haki yake ya kupata kesi inayostahiki " kwani ni mwanasiasa wa mpinzani.

Maafisa wa Uholanzi, ambao wameshawarejesha angalau washukiwa watatu wa mauaji ya kimbari ya Rwanda walofikishwa mahakamani Kigali tangu mwaka 2016, walikata rufaa hiyo iliyokatailwa na Mahakama Kuu.

Karangwa, ni afisa wa zamani wa kijeshi akiwa katika miaka yake ya sitini, anaetuhumiwa kwa jukumu lake katika mauaji ya takriban watu 30,000 wa kabila la Watutsi katika parokia ya Mugina iliyopo jirani na mji mkuu wa Rwanda, Kigali mwezi Aprili 1994.

Takriban watu 800,000 wa kabila la Watutsi na Wahutu wenye msimamo wa wastani waliuwawa wakati wa mauaji ya kimbari ya Rwanda, yaliyopangwa na utawala wa Wahutu wenye msimamo mkali na kutekelezwa kwa uangalifu na viongozi wa miji na raia wa kawaida katika jamii hiyo yenye mfumo unaoheshimiwa wa matabaka.

Karangwa tayari amenyang’anywa uraia wake wa Uholanzi kutokana na tuhuma za mauaji ya kimbari. Sasa yuko kwenye mtafaruku wa kisheria, kwani Uholanzi haimtaki lakini pia inashindwa kumrudisha Kigali

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters.

Forum

XS
SM
MD
LG