Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 04:14

Mtoro wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda, Fulgence Kayishema afikishwa mahakamani nchini Afrika Kusini


Fulgence Kayishema, mtoro wa mauaji ya kimbari ya 1994 nchini Rwanda, akiwa ndani ya mahakama ya Cape Town, Mei 26, 2023.
Fulgence Kayishema, mtoro wa mauaji ya kimbari ya 1994 nchini Rwanda, akiwa ndani ya mahakama ya Cape Town, Mei 26, 2023.

Fulgence Kayishema, mmoja wa watoro wa mwisho waliokuwa wanasakwa kwa kuhusika kwao katika mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini Rwanda, alifikishwa mahakamani mjini Cape Town nchini Afrika Kusini, siku mbili baada ya kukamatwa.

Kayishema ambaye alikuwa mafichoni kwa kipindi cha miaka 22, anakabiliwa na mashtaka ikiwemo mauaji ya kimbari na njama ya kutekeleza mauaji ya kimbari, yanayohusiana na mauaji ya zaidi ya watu 2,000 kutoka kabila la Watusti nchini Rwanda mwaka 1994, mwendesha mashtaka wa serikali amesema.

Awali, msemaji wa mamlaka ya taifa ya kuendesha mashtaka Afrika Kusini, Eric Ntabazalila, aliiambia AFP kwamba Kayishema atafikishwa mahakamani leo Ijumaa.

Alisema mwendesha mashtaka atasoma mashtaka yanayomkabili, akiongeza kuwa suala la kumpeleka nje ya Afrika Kusini halitarajiwi kujadiliwa leo.

Inspekta huyo wa zamani wa polisi wa Rwanda alikamatwa Jumatano katika shamba la zabibu huko Paarl, umbali wa kilomita 60 kaskazini mwa mji wa Cape Town, kulingana na wachunguzi wa Umoja wa Mataifa

Forum

XS
SM
MD
LG