Jaji wa mahakama hiyo Chacha Mwita ameiamuru idara ya Uhamiaji kumpa Miguna hati zake za kusafiria ili kumwezesha kurudi nchini Kenya mpaka hapo shauri lake litakaposikilizwa mahakamani juu ya uhalali wa uraia wake.
Miguna Miguna ambaye ni mwanachama wa Muungano wa upinzani Nasa na pia ni wakili alilazimishwa kupanda ndege na kurudishwa nchini Canada.
Kufukuzwa huko nchini kulifuatia kukamatwa kwake na kufunguliwa mashtaka ya uhaini kwa kuhusika na zoezi la kujiapisha kiongozi wa upinzani Raila Odinga.
Odinga ambaye ameendelea kusisitiza kuwa ndiye mshindi halali wa uchaguzi mkuu wa urais nchini Kenya uliofanyika mwaka 2017.
Wizara ya Mambo ya Ndani ilieleza kuwa Miguna alikana uraia wake wa Kenya baada ya kuchukua ule wa Canada miaka kadhaa iliyopita.